Mbio za Familia Marathon Zang’ara, Mwanake Aibuka na Ndinga
Global Publishers December 11, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kulia), akikabidhi funguo ya gari jipya aina ya Toyota Passo lenye thamani ya shs milioni 9.5 kwa mshindi wa kwanza wa KM 21 Wanawake wa mbio za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim, jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mauzo kwa Makampuni wa KP Motorz, Protas Mbeya na Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca AlphonceMwenyekiti wa Familia Marathon 2021, Francisca Alphonce (wa nne kushoto), akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe ya kutambua mchango wa udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za mwaka huu za Familia Marathon zilizotimua vumbi jijini Dar es Salaam leo zikifanyika eneo la Msasani Beach Club. KP Motorz ilitoa gari jipya aina ya Toyota Passo kwa mshindi wa pili wa KM 21 Wanawake.