
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngorongoro Dkt. Jumaa Mhina amemtangaza Mgombea wa CCM, Emmanuel Shangai kuwa Mbunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 62,017 dhidi ya wagombea wenzake wa ACT Wazalendo aliyepata kura 170 na Saimon Ngilisho wa Demokrasia Makini aliyepata kura 105.