
MVUA zinazoendelea kunyesha sehemu kubwa nchini zitaendelea kuwa chanzo cha ajali nyingi iwapo madreva hawatakuwa waangalifu na kuzingatia alama za usalama barabarani.

Moja ya ajali mbaya kutokea leo asubuhi ni ile inayohusisha gari la magazeti lilokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya.
Taarifa za awali zinasema ajali imetokea kati ya kijiji cha Mtandika na Mahenge kilichopo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa baada ya gari aina ya Hiace kuacha njia na kugonga mti na kuua watu tisa.

Picha na video zinaonesha watu wakikata mabaki ya gari ili kuokoa na kuondoa miili ya majeruhi pamoja na marehemu katika gari hiyo.
Katika Eneo la Msolwa, Bus ya kampuni ya New Force imegongana na lori nakusababisha majeruhi kadhaa. Tunaendelea kufuatilia taarifa ya kina kuhusu matukio ya ajali barabarani