
Muziki wa Rhumba wenye asili yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kongo Brazzaville, umepewa hadhi ya kuwa kwenye orodha ya urithi wa dunia katika kilele cha mkutano wa UNESCO, uliofanyika Desemba 14, 2021.
Jumla ya maombi 60 kutoka nchi mbalimbali duniani yaliwasilishwa katika mkutano huo kuwania kutambulika kwenye orodha hiyo.
Inaaminika kuwa chimbuko la Rhumba ni nchini DRC, ambapo muziki huo ulitumika kipindi cha kupigania uhuru kuwaunganisha wananchi wa nchi hizo mbili pamoja na mataifa mengine ya Afrika.
Miongoni mwa waanzishi wa muziki wa Rhumba ni pamoja na Wendo Kolosoy, Paul Nkamba, Franco, Bendi ya TP OK Jazz, Tabu Ley Rochereau na Dr Nico, wote wakitokea Kongo.
Cc; @bakarimahundu