
KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mkenya Francis Baraza ameweka wazi kuwa wameanza maandalizi ya mechi yao na Simba itakayopigwa Jumamosi hii huku lengo lao likiwa ni kupata ushindi.
“Tumeanza maandalizi ya kuhakikisha tunapata matokeo mbele ya Simba. Kikubwa tutawaheshimu maana ni timu kubwa, ni timu ambayo ina wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu pale wanapoichezea timu yao lakini hilo halitatuzuia kupambana ili tupate matokeo tunayotaka.
“Simba wasitegemee kwamba nitazuia katika mchezo huo lazima nitashambulia kutafuta matokeo hivyo pamoja na kwamba nitawaheshimu lakini mpango wangu katika mchezo huo ni kushambulia ili tusiruhusu kufungwa mara tatu mfululizo kwenye uwanja wetu wa nyumbani.”
JOHNSON JAMES