×

Xavi Amtaka Pogba Barcelona

KOCHA wa Barcelona Xavi amefunga mlango wa kutaka kumnunua nyota wa Manchester United Paul Pogba kwa sababu Mfaransa huyo hafanani na wasifu wa klabu hiyo.

Mkataba wa Pogba unamalizika mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na baadhi ya vigogo wa Ulaya, ambao ni PSG na Barcelona.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Diario Sport, Xavi amepinga kumtaka Mfaransa huyo na badala yake amemwambia rais wa klabu Joan Laporta kuelekeza mawazo yake kwingine.

Taarifa za awali zinasema wakala wa Pogba, Mino Raiola, alikutana na rais wa klabu Joan Laporta nchini Italia wiki hii ili kujadili uwezekano wa kuhama kwa wateja wake wanne, watatu kati yao wakikata kandarasi msimu ujao wa joto.

Pogba, Xavi Simons wa PSG na Noussair Mazraoui wa Ajax wote mikataba yao inaisha msimu wa joto huku mteja wa nne wa Raiola, Erling Haaland, ataweza kuhama kwa bei pungufu mara tu ya msimu utakapomalizika.

Haaland atakuwa sokoni kwa dau la pauni milioni 64 kutokana na kifungu cha mkataba wake na bado ni kipaumbele cha wababe hao wa Catalan.

Leave a Comment