×

Shoga; mwaka 2016 uwe wa kuboresha penzi lenu!

Lovely couple hugging on their bed at home

Asalaam aleykhum! Shoga yangu bila shaka unaelewa kwamba mwaka 2015 uliokuwa na matukio makubwa ya kihistoria duniani na hapa nchini kwetu kufuatia kuwepo uchaguzi mkuu uliomuwezesha Dk. John Pombe Magufuli ‘Mzee wa kutumbua majipu’ kuingia Ikulu ya Magogoni ndo unaishia.

Ni wazi kwamba unatafakari na kufanya tathmini ya mafanikio uliyoyapata katika mwaka huu au namna ambavyo hujafanya kitu chochote cha maendeleo huku ukishuhudia majirani zako wakijenga nyumba, kununua magari, kusomesha watoto nk.

Tukija upande wa uhusiano, huenda tangu tulipouanza mwaka huu wewe na mumeo, mpenzio au mchumba wako hamukuwa sawa na matokeo yake ilikuwa ni migogoro kwa kwenda mbele.

Kama hivyo ndivyo, yakupasa kuwa makini tutakapouanza mwaka mpya wa 2016 kwa sababu hakuna kitu kibaya katika maisha kama migogoro ya kimapenzi.
Nasema hivyo, kwa sababu migogoro ya mapenzi hukwamisha mambo mengi ya kimaendeleo na kiafya kwani wahusika huwa kwenye msongo wa mawazo unaosababisha afya kuzorota na hata vifo.

couple-happy-in-bed-comp-680x380Shoga, kama wewe na mwenza wako hamko sawa naamini mnaelewa kinachosababisha hali hiyo, kama ni wivu wa kupitiliza, hasira, wizi, uongo, dharau, uchafu, uchoyo, uvivu ni vyema mkajirekebisha ili muweze kufurahia penzi lenu.

Kumbuka kwamba, kama kila mmoja wenu hatakuwa tayari kujirekebisha mkiwa kama mke na mume, wapenzi au wachumba mtashindwa kukutana chumbani zaidi kwa ajili ya kujiburudisha.

Sasa kama hilo halitafanyika, wewe au huyo mtu wako atakuwa anazimaliza wapi haja zake kama si kila mmoja wenu kumsaliti mwenzake?

Shoga, kumbuka usaliti ndiyo chanzo cha kuleta maradhi hususan Ukimwi ndani ya nyumba, hebu boresheni penzi lenu mwaka mpya ili wengine wawaige naamini itakuwa poa sana. Bye!

Leave a Comment