Rapa Kanye West ameripotiwa kununua Nyumba yenye thamani ya Dola milioni 4.5 (sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 10) kando ya nyumba anayoishi aliyekuwa mke wake Kim Kardashian. Kulingana na ripoti kutoka Daily Mail, nyumba hiyo yenye vyumba 5 iko katika eneo la kipekee la Hidden Hills huko LA.
Kitendo cha Kanye kununua nyumba hiyo iliyopo katika eneo la kando ya anapoishi Kim Kardashian kumezalisha tafsiri mpya ya harakati za Kanye kujaribu kumrejea mke wake huyo waliotengana kutokana na sababu kadhaa zinazomuhusu Kanye zaidi. Licha ya ugumu unaoonekana dhahiri juu ya matumaini ya wawili hao kurudiana.
Kanye aliwahi kuweka wazi kuwa bado ana mpango wa kuiunganisha familia yake kwa mara nyingine japo ex wake huyo tayari ameshaanza mahusiano mapya na mchekeshaji Pete Davidson, Jambo linaloendelea kuyafukia matumani ya wawili hao kurudiana.
Rapa Kanye West na aliyekuwa mke wake Mwanamitindo Kim Kardashian walidumu kwenye ndoa yao kwa kipindi cha miaka 7 na kufanikiwa kupata watoto wanne.