
KLABU ya US Gendarmerie ya Djibouti imesema imepangwa kundi zuri na Simba Sc ya Tanzania hivyo wanao uhakika mkubwa wa kusonga mbele katika mashindani ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
“Tupo katika kundi lililopangwa vizuri lenye timu tatu kubwa ambazo ni Berkane iliyowahi kutwaa taji hili, Simba ambao wamekuwa wakicheza vyema katika Ligi ya Mabingwa pamoja na Asec Mimosas ambao wamekuwa wakishiriki mashindano haya.
“Malengo yetu ni rahisi tu, kumaliza tukiongoza na kufuzu hatua ya robo fainali. Tunaweza kufanya hivyo. Tunatakiwa kurudi katika mstari na kujituma pasipo kudharau taarifa yoyote muhimu,” amesema Zakariou Ibrahim, Kocha Mkuu US Gendarmerie.