
Kiungo Mkongwe Deusi Kaseke huenda akaguswa na maamuzi ya Benchi la Ufundi la Young Africans ya kumtoa kwa mkopo mmoja wa viungo wa klabu hiyo.
Usajili wa kiungo Denis Nkane unalazimisha kufanywa kwa maamuzi ya kiungo mmoja kuondoka klabuni hapo kwa mkopo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo La Usajili.
Imefahamika kuwa Kaseke ambaye hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ataguswa na uamuzi huo ambao umeshapewa baraka na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.