
Nyota wa kikosi cha Liverpool Sadio Mane na mlinda lango namba moja wa Chelsea Eduardo Mendy wamesafiri pamoja kurejea nyumbani Afrika kwaajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Senegal tayari kwa michuano ya AFCON.
Nyota hao walicheza kwenye mchezo wa jumapili wa ligi kuu soka nchini England Chelsea walipowaalika Liverpool.
Senegal ni wanafainali waliopita wa michuano ya AFCON walipopoteza kwa kufungwa na Algeria timu zilizokuwa kwenye kundi moja na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwenye michuano hiyo.