×

Marafiki wasishike ndoa yako, utajuta!

Vanessa3HABARI zenu wapenzi wasomaji wa kona hii, kama mnaendelea vema nashukuru kwa hilo, leo kungwi nimekuja kuwaasa akina mama wenye ndoa ambao mnajisahau kwa kudanganywa na marafiki.

Kumbuka marafiki wengine huwa hawapendi mema ya rafiki zao, shtuka mapema bibi ukiona mwenendo siyo achana na marafiki wabaya.Ndoa ni daraja, kama zima unatakiwa kulivuka, kama bovu pia unatakiwa kulivuka, kama ni bovu lifanyie ukarabati kwa sababu unatakiwa kuvuka.

Kwenye ndoa kuna misukosuko mingi ndiyo maana ikaitwa safari ndefu, unaweza kujikuta unakutana na daraja bovu lakini ni jukumu lako kulipita ili ufikie safari yako, hivyo kwako wewe mwanandoa ni lazima kuhakikisha unavuka, utakutana na vikwazo vingi, kukosa, kupata ni hali ya kawaida ambayo ipo na lazima ukabiliane nayo kama ulivyoahidi siku uliyofunga ndoa kuwa utaishi katika ndoa yako kwa shida na raha.

Kuna baadhi ya wanawake pale waume zao wanapokosa hata mtaa wa saba utapata taarifa, kumbuka hakuna mkamilifu isipokuwa Mwenyezi Mungu, kwa nini usiweke siri za nyumba yako mpaka ukazitangaze?

Leo utachukua tatizo utamshtakia shoga, huyo shoga mumeo anamtaka atakushawishi kwa namna yoyote ile utajikuta unamuacha na baada ya siku utasikia kakaa yeye.

ashosti wa siku hizi hawana maana, angalia mwenye manufaa na wewe lakini pia usitoe siri zako kamwe kwa shosti wako, atakuliza bibi afu utabaki kusema ungejua.

Ongeeni mambo mengine ya maendeleo lakini si udhaifu wa mumeo kwani mwanamke asiyekuwa na siri ni mjinga anayeibomoa ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine tena.

Leave a Comment