×

Mayele: Tunawapiga Azam

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa wanahitaji kupata ushindi kwa hali yoyote dhidi ya Azam ili waweze kutinga katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ambayo ni fainali.

 

Mayele jana Jumapili alitua visiwani Zanzibar akitokea Dar ambako aliingia Jumamosi usiku akitokea kwao DR Congo hivyo leo atakuwepo Uwanja wa Amaan wakati Yanga ikiumana na Azam FC kwenye nusu fainali ya kwanza saa 10:15 jioni.

 

Mayele ni kati ya wachezaji watano wanaoongoza kwa mabao Ligi Kuu Bara ambapo kila mmoja amefunga matano.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayele alisema kuwa, malengo yao kama timu ni kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano hiyo jambo ambalo ameahidi kupambana sambamba na wachezaji wenzake kwa ajili ya timu ili kufanikisha jambo hilo.

 

“Malengo ya timu katika michuano hii ni ipo wazi ni kutetea ubingwa huu, hatuwezi kuutetea ubingwa kama tutashindwa kutinga katika hatua inayofuata ya michuano hii hivyo kwa kuwa kwa sasa tupo katika hatua ya nusu fainali basi tunatakiwa tufike fainali.

 

“Baada ya kufika fainali sasa hapo ndio tunatakiwa kuanza kufikiria kuhusu ubingwa lakini kama hatutafikia huko basi tutakuwa tumefeli, kuhusu kuwafunga Azam FC ilitokea kwenye ligi hivyo sitaki kusema kitu au kuweka ahadi ya kuwafunga Azam FC lakini matarajio yangu ni kuisaidia timu,” alisema Mayele.

Leave a Comment