
KOCHA Msaidizi wa Yanga Mrundi, Cedric Kaze amepanga kukitumia kikosi chake chote cha kwanza katika mchezo wao dhidi ya Azam FC utakaopigwa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Timu zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi unaotarajiwa kupigwa saa 10:15 jioni.
Hiyo ikiwa siku chache tangu wachezaji wake wajiunge na kambi ya timu hiyo ambao ni Khalis Aucho, Yannick Bangala, Said Ntibanzokiza kocha akiwa yeye mara baada ya kukabidhi kikosi hicho.
“Itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kusonga mbele. Vijana wapo vizuri na morali kubwa ya ushindi, hivyo ninapata matumaini ya kulitetea kombe letu.
“Azam wamebadilika sana kiuchezaji tofauti na walivyokuwa kwenye ligi hivyo tutaenda mbele yao kwa tahadhari kubwa ili kuusaka ushindi kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo.
“Katika mchezo huo hatautumia kujaribu wachezaji na badala yake atakitumia kikosi cha kwana ambacho walikuwa wakikitumia katika ligi mara baada ya Aucho, Bangala na Saido kuripoti kambini,” alisema Kaze. ‘Saido’ ambao wote tayari Zanzibar.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema kuwa siyo mchezo mwepesi kwao dhidi ya Azam, hivyo amepanga kuwatumia wachezaji wote muhimu na tegemeo katika kikosi chake.
Kaze alisema kuwa kurejea kwa wachezaji hao kutampa nafasi ya kupanga kikosi kitakachompa ushindi katika mchezo huo na kufuzu fainali ya michuano hiyo. Alisema kuwa malengo yao makubwa ni kulitetea kombe hilo ambalo walilichukua, mwaka jana.
MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
Mwaka Bingwa Wa pili
2007: Yanga Mtibwa
2008: Simba Mtibwa
2009: Miembeni KMKM
2010: Mtibwa Ocean View
2011: Simba Yanga
2012: Azam Jamhuri
2013: Azam Tusker
2014: KCCA Simba
2015: Simba Mtibwa
2016: URA Mtibwa
2017: Azam Simba
2018: Azam URA
2019: Azam Simba
2020: Mtibwa Simba
2021: Yanga Simba (P)
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam