×

Fahyma Adaiwa Kuwa na Mimba Ya Rayvanny

BABY mama wa msanii Rayvanny, Fahyma ameendelea kuonesha ishara kwamba huwenda amerudiana na jamaa huyo baada ya kudaiwa kubeba mimba yake.

 

Fahyma anadaiwa kuwa amebeba ujauzito wa mtoto wa pili, lakini inafahamika kwamba hakuna mwanaume mwingine aliye karibu yake zaidi ya Rayvanny ambaye amezaa naye mtoto mmoja.


Mrembo huyo ameendelea
kuposti picha zikionesha tumbo lake likionesha kwamba ni mjamzito na siyo kwamba
ameshiba ubwabwa huku
akipokea pongezi kutoka kwa mastaa mbalimbali akiwemo Muna Love.


Alichokifanya Fahyma
ni kuwashukuru wote wanaompongeza kwa kuwa mjamzito. Inafahamika kwamba, Fahyma na Rayvanny walitengana mwaka jana baada ya jamaa huyo kutimkia kwa mrembo
Paula Kajala ambaye kwa sasa
yupo masomoni nchini Uturuki.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

SAKHO ATUMA SALAMU YANGA, KISA SIMBA MANARA ASHINDWA KUJIZUIA, YANGA CHALI | KROSI DONGO

Leave a Comment