×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Habari
  3. Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi

Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi

Global Publishers January 15, 2022 0 Comments
SHARE THIS:

Kesi ya mauaji inayomkabili Timothy Gitonga mwenye umri wa miaka 30, anayetuhumiwa kumuua bibi yake, Journes Kiringa mwenye umri wa miaka 80, imeshindwa kusikilizwa kufuatia mtuhumiwa huyo kuzidiwa na maradhi akiwa kizimbani.

 

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Embu, nchini Kenya ambapo mtuhumiwa alipoingizwa mahakamani, alianza kulalamikia maumivu makali aliyokuwa akiyahisi, jaji akaamuru kesi iendelee lakini mtuhumiwa aliendelea kulalamikia maumivu makali huku akionesha kuzidiwa.

 

Kufuatia hali hiyo, Jaji Tony Kwambai aliamua kusitisha usikilizwaji wa kesi hiyo na kuagiza mtuhumiwa apelekwe katika Hospitali ya Embu na baada ya matibabu arejeshwe katika Kituo cha Polisi Itabua kisha apelekwe tena mahakamani hapo ifikapo Januari 17, mwaka huu.

 

Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kudaiwa kumshambulia bibi yake na kumuua huku akimjeruhi vibaya babu yake, Jamleck Wamai ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Embu.

 

Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Rungana, Nembure ambapo sababu za tukio hilo hazijafahamika na baada ya kutenda ukatili huo, mtuhumiwa alitoroka kabla ya kukamatwa na polisi.

SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

Jeshi la Polisi Lafafanua Ukamatwaji wa Wachokonozi – Video - Global Publishers GLOBAL TV ONLINE

Jeshi la Polisi Lafafanua Ukamatwaji wa Wachokonozi – Video

June 22, 2025
Wananchi Waangusha Maombi Maalum Dhidi ya Mauaji ya Watoto Njombe - Global Publishers HABARI

Wananchi Waangusha Maombi Maalum Dhidi ya Mauaji ya Watoto Njombe

February 11, 2019
Mameneja 9, Mkurugenzi Mstaafu Dawasco Watumbuliwa - Global Publishers HABARI

Mameneja 9, Mkurugenzi Mstaafu Dawasco Watumbuliwa

March 12, 2016
Jiunge Na Huduma Mpya kutoka Halotel - Global Publishers HABARI

Jiunge Na Huduma Mpya kutoka Halotel

November 14, 2016

Leave a Comment Cancel reply

You must be logged in to post a comment.



DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services