×

Qatar Airways Yaadhimisha Miaka 15 ya Safari Zake Dar

Shirika la ndege la Qatar mwezi huu linaadhimisha miaka 15 ya mafanikio tangu ilipoanza safari yake ya kwanza kati ya Doha na Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 9 Januari, 2007.

 

Qatar Airways kwa mara ya kwanza ilizindua huduma za ndege zake Tanzania kwa safari mbili kila wiki mnamo Januari 2007, ambayo sasa imeongezeka hadi safari 19 kwa wiki zinazoendeshwa na mchanganyiko wa ndege za Boeing 787 na Airbus A320.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais wa Qatar Airways, Afrika, Hendrik du Preez, alisema siku zote wamekuwa wakijivunia kuitumikia Tanzania wakiiunganisha na mtandao wao wa kimataifa.

 

“Maadhimisho yetu ya miaka 15 yanaimarisha zaidi uhusiano wetu na Tanzania na uwezo mkubwa ambao njia ya Dar es Salaam imeonyesha kwa miaka mingi.

 

Hii ilikuwa hasa katika kilele cha janga la Uviko19, wakati Dar es Salaam ilikuwa na mahitaji makubwa. Tunatazamia miaka mingi zaidi ya kuwaunganisha wasafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kujionea utamaduni na wanyamapori wa kipekee wa Tanzania,” alisema Bw Preez.

 

Qatar Airways sasa inaendesha safari za ndege mbili kila siku hadi Doha kutokea Dar es Salaam huku QR1348 ikiondoka saa 6 usiku na QR1499 ikiondoka saa saa 5 asubuhi, pamoja na safari moja ya kila siku ya QR1476, bila kujumuisha ile ya Jumanne na Alhamisi inayoondoka saa 8 mchana.

 

Dar es Salaam ikiwa ni sehemu yenye historia na utamaduni, inajulikana kwa muziki na vyakula vilivyojaa viungo kama ilivyo historia yake ya baharini na bandari nzuri. Kama mojawapo ya majiji yanayokuwa kwa kasi zaidi Afrika Mashariki, wageni wanaotembelea Dar es Salaam wanaweza kutazama maonyesho ya sanaa au kwenda kwenye matembezi kwenye fukwe zake zenye mchanga mweupe.

 

Qatar Airways inaendelea kusaidia wasafiri kwa ajili ya biashara na utalii, na kuwaruhusu kuunganishwa maeneo wanayopenda kupitia mtandao unaopanuka kote Ulaya, Asia na Marekani.

Qatar Airways Cargo inasaidia biashara ya bidhaa kama vile samaki, nyama na maua kwenda sehemu mbali mbali kwenye mtandao wa Qatar Airways kama Hong Kong, Qatar na Uholanzi, na uagizaji wa bidhaa vya teknolojia na dawa.

 

Shirika la ndege la Taifa la Qatar linaendelea kujenga upya mtandao wake, ambao kwa sasa unapatikana katika vituo zaidi ya 140 ulimwenguni, vikiwemo Kilimanjaro na Zanzibar.

 

Huku safari nyingi za ndege zikiongezwa kwenye vituo muhimu, Qatar Airways inatoa masharti rahisi ya kuweka nafasi kwa abiria, na hivyo kurahisisha kubadilisha tarehe zao za safari.

 

Wateja wanaweza kunufaika kutokana na masharti rahisi ya kukata ambayo yanatumika hadi Mei 2022.
Kama shirika la ndege lililoshinda tuzo nyingi, Qatar Airways hivi karibuni ilitwa tuzo la ‘Shirika Bora la Ndege Ulimwenguni’ katika Tuzo za Shirika la Ndege la Dunia, zinazosimamiwa na shirika la kimataifa la ukadiriaji wa usafiri wa anga la Skytrax.

 

Kitovu cha shirika hilo la ndege, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad (HIA), ulitambuliwa hivi majuzi kama ‘Uwanja Bora wa Ndege Duniani 2021’, pia ulioorodheshwa katika nafasi ya kwanza katika Tuzo za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Skytrax 2021.

Leave a Comment