×

Ukimtaka Adele, Jipange

STAA wa muziki kutoka nchini Marekani ambaye ni mzaliwa wa uingereza, Adele Laurie Blue Adkins ‘Adele’ ameripotiwa na vyombo mbalimbali kuwa ulipwa kiasi cha fedha za Kimarekani dola $700,000 kwa shoo ya siku moja.

 

Taarifa hizo zimeibuka baada ya kulipwa katika shoo moja iliyofanyika huko Las Vegas Nevada huko Marekani, kiasi cha pesa hicho kinakadiriwa ni sawa na Bilioni 1.6 za Kitanzania.

 

Inaelezwa shavu hilo uambatanishwa na chumba atakacholala chenye thamani ya fedha za Kimarekani $ 30,000 ambazo ni sawa na milioni 70 za Kitanzania.

 

Adele kwa sasa anatamba na albamu yake mpya aliyoingiza sokoni mwaka jana inayokwenda kwa jina la 30 Album ambayo bado inaendelea kufanya vizuri ndani ya wiki sita tu sokoni.

 

Imeripotiwa kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 33 anategemewa kuwa msanii wa kike anaelipwa pesa nyingi zaidi kwa shoo moja kwani hivi karibuni atalipwa takribani dola milioni 1 ambazo zinatokana na mauzo ya tickeki pekee kabla ya mauzo ya bidhaa zake kama nguo na albamu.

Adele ana shoo 24 katika ukumbi wa kifahari wa Caesars Palace kama sehemu yake shoo zake za ‘Las Vegas Residency’.

 

Ticket moja inauzwa kwanzia Tsh milioni 3 mpaka Tsh milioni 40. Las Vegas Residency ni tukio la kipekee la msanii kupewa zaidi ya show 10 kwenye ukumbi mmoja kila weekend kutokana na wingi wa mashabiki na soko lake.

Leave a Comment