
SUPASTAA kutoka pande za Nigeri, Joseph Akinwale Akinfenwa-Donus ‘Joeboy’ amefanikiwa kutimiza streams milioni 100 katika mtandao wa muziki wa Boom Play.
Sasa JoeBoy ameunagana na wasanii wengine wakubwa nchini Nigeria waliofikia kiwango hicho cha Streams akiwemo Fireboy DML, Burna Boy na Olamide wenye Streams zaidi ya milioni 100 sasa.
Streams za JoeBoy zilipanda zaidi mwezi Februari 2021, baada ya staa huyo wa AfroPop kutoa albamu yake ya kwanza ‘Somewhere Between Beauty & Magic’ iliyogonga streams milioni 60.
Kingine ni ile ngoma yake mpya ‘Sip (Alcohol)’ imekuwa rekodi iliyopata Streams nyingi zaidi ikiwa na stream milioni 50. Kwa sasa Alcohol ni nyimbo ya tatu iliyosikilizwa zaidi BoomPlay kwa mwaka 2021.
BoomPlay wanasema nyimbo za JoeBoy zinasikilizwa zaidi katika nchini 163 duniani kupitia mtandao huo mkubwa wa muziki duniani.