×

Janjaro: 2022 ni Mwaka wa Kuwasaidia Wachanga

RAPA maarufu Bongo, Abdulaaziz Chande ‘Dogo Janja’ amesema kuwa kwake yeye mwaka 2022 ni mwaka wa kuwassapoti wasanii wachanga ikiwa ni kurudisha fadhira kwa jamaii kwa kile ambacho amesema kuwa ni muda wakuwapa wasanii wapya nafasi.

 

Janjaro amesema; “Katika maisha yangu ya muziki nadhani historia yangu ya mimi kutoka kila mtu anaijua, so nadhani pia huu ni muda wa mimi kurudisha katika jamii, mwaka sitarajii kufanya mimi sana, lakini nitakuwepo nyuma ya huu muziki, kwa hiyo nadhani ni muda wakuwapa nafasi watu wapya wenye vipaji.

“Tunaweza kuwaombea masikio kwa sababu tunaamini wakisikika watazingatiwa, hata #Madee huwa namwambia kuwa natamani na mimi siku moja nirudishe katika jamii so huu umekuwa ni muda mzuri sana na uzuri kuna baraka kwa mabraza hivyo ni kitu kizuri sana,” amesema Janjaro.

Leave a Comment