×

Kikaangoni Leo… Halima Yahya ‘Davina’ Agoma kutoa siri ya kuachana na mumewe

Davina_1.jpgNI siku nyingine tena kwenye kolamu hii inayowakutanisha na mastaa mbalimbali Bongo na kufunguka mambo kadha wa kadha katika jamii inayowazunguka, kuhusiana na maisha yao kiujumla.

Leo katika kona hii, tunaye msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ ambaye amefunguka maswali mengi kama ifuatavyo;

Msomaji: Hadi sasa sijapata jibu ni kitu gani hasa kilichokufanya uachane na mumeo, hujui ndoa ni kitu cha kujivunia?

Davina: Hili suala la kuachana na mume wangu ni siri nzito ambayo tunaijua mimi na yeye, ujue kwenye ndoa kuna mambo mengi, yapo yanayovumilika na mengine huwezi kuyavumilia.

Msomaji: Nakufuatilia tangu kipindi cha nyuma enzi hizo unafanya maigizo kwenye runinga katika Kundi la Kaole upo fiti kwenye kazi zako, lakini mbona sasa umekauka sokoni, kwa nini unatunyima uhondo mashabiki wako?

Davina: Soko limeshuka sana si sawa na kipindi cha nyuma, kingine filamu zetu hazina ubunifu utakuta mtazamaji akianza tu kutazama anatabiri filamu nzima itakavyokuwa.

Msomaji: Hivi ni kwa nini mastaa wengi mnashindana kununua magari na si nyumba, vipi wewe umeshabahatika kumiliki mjengo?

Davina: Mimi sipo katika huo ushindani wa magari, naishi kiuhalisia siyo kwa mashindano, kuhusu mjengo hiyo ni siri yangu siko tayari kuanika hilo.

Msomaji: Ningependa kujua mbali na sanaa unajishughulisha na nini?

 Davina: Nafanya biashara mbalimbali zikiwemo bidhaa za wanawake na kadhalika, maana sanaa yenyewe kufanya ndiyo hivyo kwa msimu.

Msomaji: Kwa nini wasanii wengi Bongo wanapenda kufeki maisha, wengine pesa hawana magari wanalazimika kukodi Bajaj kila siku na wengine wanalazimisha kusomesha watoto shule za gharama?

Davina: Tatizo ni kwamba mashabiki wetu wanajua sisi tuna pesa sana ndiyo maana mtu unalazimika kuishi kutokana na hadhi ya jina lako.

Leave a Comment