The House of Favourite Newspapers

Mama: Tayari Zuchu Amelipiwa Mahari

0

BI KHADIJA Kopa ni Malkia wa Taarab Afrika na ni mama wa malkia mwingine wa Bongo Fleva, Zuchu ambaye
amesainiwa kwenye Lebo
ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz anayesemekana ni mpenzi wake kwa sasa na
wanapanga kufunga ndoa.


Mapema tangu asainiwe
kwenye lebo hiyo, siku ile ya Aprili 8, 2020, kulianza kusikika tetesi kuwa huwenda Zuchu akawa na uhusiano wa ziada; yaani zaidi ya kazi na Diamond. Hii ni kwa sababu wawili hao wamekuwa na ukaribu wenye viulizo hasa baada ya kunaswa hotelini mwezi uliopita huku Bi Khadija akisema tayari Zuchu amelipiwa mahari bila kutaja mtu aliyemlipia.

 

Kauli hiyo ya Bi Khadija inakuja siku chache baada ya Zuchu kuthibitisha kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu aliyempatia zawadi ya mdoli mkubwa.


“Mimi sina taarifa
kwamba anaolewa na Diamond, lakini ninachojua tayari (zuchu) amelipiwa mahari…”
Anasema Bi Khadija bila
kutaja ni mwanaume gani aliyemlipia Zuchu mahari.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply