×

Soggy Dogg bwana, eti Nimemis Kukabwa!

SOGGYDOGY-620x400Anselm Tyrphone Ngaiza ‘Soggy Dogg’

Stori: Andrew Carlos
DUUHH!! BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma, staa mkongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Anselm Tyrphone Ngaiza ‘Soggy Dogg’ anatarajia kuja na ujio mpya atakaouita Nimemis Kukabwa.

Soggy Dogg aliyewahi kubamba na Ngoma ya Kibanda cha Simu alisema kuwa gemu ya muziki wa sasa ni nyepesi na kwamba ni kitendo cha kuchora ramani unaimba nini na wakati gani unatakiwa kutoa ngoma mpya.

“Siku hizi gemu nyepesi sana. Nipo njiani kuibuka na Ngoma ya Nimemis Kukabwa ambayo ndani yake ni full vituko. Ngoma imepikwa na T.Touch wa Free Nation,” alisema Soggy.

Leave a Comment