×

Simba Kukiwasha na Kagera Sugar Kaitaba Leo

UONGOZI wa Simba umesema kuwa wana furaha kubwa kwenda kucheza Bukoba kwenye uwanja wa kisasa
na wenye hadhi yao dhidi ya
Kagera Sugar.


Timu hizo leo Jumatano
zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara majira saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba mkoani Kagera.


Uwanja wa Kaitaba wenye
nyasi bandia, ni kama ule wa Simba wanaoutumia katika mazoezi yao uitwao Simba Mo Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa kiwanja hicho kitawapa fursa wachezaji kuonesha kiwango bora ambacho Wanasimba wanakitaka.

 

Ally alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia mia moja baada ya jana asubuhi kusafiri kwa ndege kuelekea Bukoba tayari kwa mchezo huo.

“Kikubwa tunachofurahia ni kwamba tunawenda Bukoba kucheza katika kiwanja chenye hadhi yetu, kiwanja ambacho kinawapa fursa wachezaji wetu kuonesha ubora wao.

“Hakuna asiyefahamu uwezo wa wachezaji wetu walioipa ubingwa wa ligi kwa miaka minne mfululizo siyo kitu kidogo.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

MASTAA YANGA WACHOTA MIL 265, YAAHIDI UBINGWA NBC, JEURI YA SiMBA HAWATISHIKI NA POINT…

Leave a Comment