×

Paula: Kuna Maisha Baada ya Mapenzi

MAPENZI ni ya muhimu maishani mwa kila mmoja, hasa wakati umempata mtu akufaaye maishani
mwako.

 

Kuna baadhi ya watu ambao wamekataa tamaa kwa ajili ya mapenzi na kuiambia mioyo yao ifanye kazi ya
kusukuma damu na
wala siyo kupenda.

 

Paula Kajala ni binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja na prodyuza wa Bongo Fleva, P Funk Majani ambaye ni maarufu mno mitandaoni. Hii ni baada ya kuwa mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny ambao uhusiano wao ukisemwa mno mitandaoni.

 

Paula na Rayvanny wamekuwa wakivuma mitandaoni baada ya uvumi kuibuka kwama wawili hao wameachana.

 

Wawili hao hawajaweka wazi kama wameachana, ilihali wameacha kwa mujibu wa mitandao ya kijamii baada ya kila mmoja kufuta picha zao wakiwa pamoja.


Katika
kusherehesha kinachozungumzwa kwamba huwenda wameachana, Paula ameibuka na kauli iliyoashiria kuna tatizo akiwataka wafuasi wake kuendelea na maisha yao hata baada ya mapenzi.

 

Paula anawashauri; “Kuna Kuna maisha baada ya mapenzi…” Hata hivyo, habari za ndani zinadai kwamba, huwenda kuachana kwa Paula na Rayvanny ni kiki kwani wasanii wengi wamezoea kutumia mapenzi yao kama kiki ili kazi zao zisambae na wasikauke midomoni mwa watu.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave a Comment