
MTU mmoja amepigana vita vikali dhidi ya mamba katika harakati za kuokoa wavu wake wa kuvulia samaki nchini Msumbiji.
Joao Armando ,35, kwasasa yuko hospitalini akiuguza jeraha akiwa katika hatari ya mkono wake mmoja kukatwa baada ya mkono wake wa kushoto kuumwa na mamba huyo mkubwa , mguu wake wa kulia pia ulijeruhiwa.
Alikuwa akivua samaki katika mto Shire , ambao hupeleka maji yake katika mto Zambezi , wakati alipomuona mambo huyo anaukatakata wavu wake. Akiwa ufukweni alijaribu kuuvuta wavu huo, lakini mamba huyo alimvuta ndani ya maji na hapo ndiposa vita vikali vikaanza.
‘’Mamba huyo alinivamia, nikajaribu kumuua’’, alisema bwana Armandokwa lugha ya Csena inayozungumzwa eneo hilo.
Katika vita hivo, mamba huyo alimuingiza mvuvi huyo ndani ya maji ,’’ nilipiga kelele kupata usaidizi na muda mfupi nikaokolewa na watu waliokuwa karibu’’.
Daktari wa upasuaji aliyemtibu alisema kwamba alikuwa amepoteza fahamu alipowasili katika kliniki katika eneo la Mortumbala. Armando anahamishwa katika hospitali nyengine katika mji wa Quelimane kwa matibabu zaidii.