
Mwanaharakati kutoka nchini Poland, Malgorzata Dec amefanya ziara maalum katika ofisi za Kampuni ya Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es salaam.

Mwanaharakati huyo ambaye amefanya ziara na kutembelea vitengo mbalimbali vya ofisi za global ikiwemo idara ya habari ya magazeti pendwa ambayo inazalisha gazeti la Ijumaa pamoja na ya michezo yakiwemo Championi na Spoti Xtra.

Mbali na hapo ametembelea ofisi za Global Tv Online pamoja na Global Radio huku lengo la ziara hiyo ikiwa ni kujifunza kwa nini watu wa Afrika wamekuwa na furaha wakati wote.