
SIKU ya kumbukumbu ya kuzaliwa (birthday) ya mtangazaji Millard Ayo (Mtu wa Nguvu) wiki iliyopita, mtangazaji mwenzake Meena Ally aliibua gumzo kiasi cha baadhi ya wafuasi wao kuhoji kama wao ni kitu na boksi (wapenzi)?
Inafahamika kwamba, Millard na Meena Ally ni marafiki walioshibana mno, lakini safari hii wameibua mjadala ulioshiba.
Meena Ally alimuandikia Millard ujumbe huu mzito; “Happy birthday to my best friend foreverrrr @millardayo. My brother, my ride or die, my side kick on a side, partner in crime, my nigga my nigga my Geeeee!!
“Ahsante kwa miaka yote uliyochagua kuwa rafiki yangu, nimejifunza mengi sana kwako na naendelea kujifunza kila siku!
“When all fails, I know I will pass with you! Kiumbe mwenye nusu ya moyo wangu chiiiii, Mungu aendelee kukubariki miaka mia, Dam dam milele, Love you always…”
Kwa upande wake, Millard akajibu; “Thanks a lot my nigga my nigga my nigga my Geeeee!!!!!!!! mpaka mwisho, mwisho kabisa yaani…”
Gumzo hilo linakuja miezi kadhaa baada ya Millard kudaiwa kufunga ndoa jijini Arusha, lakini wengine wakidai haikuwa ndoa bali jamaa huyo alikuwa akirekodi tangazo.