×

Ndoa ya Makabila Kimewaka ‘Mawifi Wakiwasha’

Makabila
MAPEMA tu ndoa ya msanii Dulla Makabila na mkewe Rahima, imeanza kuwatoa jasho.
Mawifi yaani baadhi ya dada wa Mkabila wanadaiwa kuanza kuisagia kunguni ndoa hiyo kwa kile kinachotajwa kuwa ‘hawamwelewi wifi’ yao.

 

Hata lile sakata la mwanamke kujitokeza na kusema kuwa, ana mimba ya Makabila imedaiwa kuwa, ni silaha iliyokuwa inatumika kuisambaratisha ndoa hiyo mapema.

 

Lakini, wanandoa hao ni kama wameshtukia mchezo huo mchafu ambapo jana usiku walikiambia kituo kimoja cha radio kuwa, ndoa yao iko imara.

 

Aidha, mke wa Makabila alimwambia mwanamke huyo “mjamzito” kuwa yeye yuko tayari kulea hiyo mimba na mtoto akipatikana atasimamia upimaji vinasaba ‘DNA’ na kumtaka aache kuhangaika na Makabila.

 

“Tunayo nyumba kubwa, akitaka anaweza kuja tukampa chumba na akizaliwa mtoto na kuonekana ni wa Dulla nitamlea, tena vizuri sana, mimi ni mwanamke hata sasa nalea watoto wengi,” amesema Rahima katika mahojiano hayo.

STORI NA RICH MANYOTA | GPL

Leave a Comment