
HABARI nzuri kwa Wanayanga ni kuwa baada ya siku 14 tu watapata kuona maufundi ya kiungo wao mshambuliaji, Denis Nkane ambaye alikuwa nje kwa sababu ya majeraha.
Kiungo huyo kwa muda hakuwa dimbani baada ya kupata majeraha ya kinena kwenye Kombe la Mapinduzi lililofanyika Januari, mwaka huu visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dokta wa Yanga, Youssef Mohammed alisema kiungo huyo amebakiza wiki mbili pekee kabla ya kurudi dimbani huku kukiwa na wachezaji wengine nao wakianza mazoezi.
“Kuna baadhi ya wachezaji kama Feisal ambao walikuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi lakini kwa upande wa Nkane (Denis) bado ni majeruhi.
“Nkane alikuwa na jeraha la kinena ambalo lilipaswa kumuweka nje kwa muda wa mwezi lakini mpaka sasa amebakiwa na wiki mbili kwa ajili ya kurejea uwanjani.”
LEEN ESSAU, Dar es Salaam