The House of Favourite Newspapers

Simba Yamchimba Mkwara Bernard Morisson

0

UNAAMBIWA KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morisson, mpaka Feb 8, 2022 hakuwa ameandika barua ya maelezo baada ya kutakiwa kuandika kujibu makosa ya kinidhamu yanayomkabili huku uongozi ukimchimba mkwara kama akiendelea kuchelewa atapelekwa kamati ya nidhamu.


Kiungo huyo ambaye
alitimka nchini kwenda kwao Ghana ikiwa ni muda mfupi baada ya kusimamishwa alitua
nchini usiku wa kuamkia jana
Jumanne na uongozi wa Simba umemkumbusha kuwa anatakiwa kuandika barua
hiyo la sivyo hatocheza
mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas Jumapili hii.


Morrison ambaye
mpaka sasa hayupo kambini baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kile kilicholezwa kuwa mtovu wa nidhamu, kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa kurudi
kuichezea Yanga.


Hivi karibuni,
wakati Simba ikitangaza kumsimamisha nyota huyo raia wa Ghana, taarifa yao ilibainisha kwamba
lazima aandike barua ya maelezo
kwenda kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.


Lakini inaelezwa kuwa, kiungo
huyo yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa
miaka miwili ya kuichezea Yanga
wenye thamani ya Sh 230Mil.


Akizungumza na Championi
Jumatano, Meneja Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Kwanza kabisa ijulikane kuwa Morrison ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba, yeye amerejea nchini leo (jana) usiku akitokea kwao Ghana.


“Mpaka leo (jana) asubuhi,
Morrison bado hajatuma barua ya aina yoyote ile ya kujieleza makosa yake kwa uongozi
labda hapo baadaye
huenda akatuma barua hiyo.


“Kama hataweza
kutuma haraka barua hiyo na kamati kuamua hukumu yake, basi ataukosa mchezo wetu ujao dhidi ya Asec Mimosas,” alisema Ahmed na kuongeza kuwa: “Suala lake limefikia katika hatua hiyo kwa hivi sasa,
lakini
kama akiendelea kugoma kuandika barua basi litapelekwa katika kamati ya nidhamu ya timu Simba
kwa ajili ya
kumjadili kabla ya maamuzi mengine kuchukuliwa.”

SORI: WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MVUTANO MKALI BUNGENI, SAKATA LA NGORONGORO – “NG’OMBE WALIOPO NI WA MABEBERU” SALOME MAKAMBA

Leave A Reply