×

Washindi wa Droo ya Tatu ya Baba Lao Waondoka na Mtonyo

Wale washindi sita waliopatikana kupitia droo ya tatu ya bahati nasibu ya Jishindie Gari na Championi au Baba Lao hatimaye wamekabidhiwa fedha zao leo Ijumaa katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori Dar.

 

Washindi hao walikabidhiwa fedha hizo na Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers Anthony Adam na tukio hilo lilirushwa moja kwa moja kupitia Global TV Online. Droo hiyo ilichezwa Ijumaa ya wiki iliyopita katika ofisi hizo hizo za Global Publishers.

Washindi hao ambao walitingwa katika ofisi hizo ni, Andrew Mbanga, Amos Paul, Fadhil Salum na Tanzan Shams na Jumanne Shaban ambao wote wanatoka Dar na watakabidhiwa fedha shilingi 50,000 na tisheti zenye nembo ya Baba Lao.

 

Anthony alisema kuwa wamekamilisha mchakato wa kutoa zawadi hizo na hiyo ni ishara kuwa wamefumga rasmi harakati zote za kuchezesha droo ndogo na sasa wanachokiangalia ni kujua nani atafanikiwa kuondoka na Toyota FunCargo, mwezi ujao.

 

“Hawa washindi ambao wapo hapa ofisini wamepatikana hapa Dar es salaam, ndiyo maana imekuwa rahisi kwao kuja na kuchukua zawadi zao, lakini yule wa Tanga tumeshamtumia pia.

 

“Hii ni ishara kuwa tumefunga kabisa mchakato wote wa droo ndogo, sasa tunajiandaa kuitangaza droo kubwa ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao, watu waendelee kujaza kuponi kwa wingi,” alisema Anthony.

 

Kwa upande wa washindi hao kila mmoja alipata nafasi ya kuzungumzia namna ambavyo alipokea kitita hicho na kila mmoja akitamba kuwa hawatoacha kujaza kuponi hadi mwisho kwa kuwa wanahitaji kushinda gari.

 

“Mimi niishukuru sana Global kupitia magazeti yake ya Championi, sikuwa na uhakika kama ningefanikiwa kushinda hii fedha, sasa nimepata nguvu nyingine ya kuendelea kushiriki hadi nishinde gari tena awamu hii nikishirikiana na mke wangu,” alisema mzee Andrew Mbanga.

Naye Amos Paul alisema kuwa: “Namshukuru Mungu kwa ushindi huu ambao
sikuwahi kutarajia kama ningeshida, naamini nikizidisha maombi nitafanikiwa
kushinda kwenye droo kubwa ambayo naweza kujipatia gari.”

Mara baada ya washindi wote kuzungumza Anthony alitumia nafasi hiyo pia kuwasititiza wasomaji wa Championi kuwa kadri wanavyonunua magazeti ya Championi na kujaza kuponi ndiyo wanajiweka katika mazingira mazuri ya kushinda gari.

 

Hivyo ni vyema wakaendelea kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa gari ipo kwa ajili ya mtu yeyote ambaye atakuwa na juhudi ya kujaza kuponi kwa wingi.

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

 

JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

Na Issa Liponda.

Leave a Comment