×

Polisi Yateketeza Bia

Polisi wenye msimamo mkali wa dini katika eneo la Kano nchini Nigeria wameteketeza chupa milioni nne za bia katika msako mkali wa pombe ambapo chupa hizo zilisagwa ardhini na tingatinga mbele ya umati wa Watu waliokuwa wakishangilia kwa kusema “Allahu Akbar” (Mungu ni mkubwa).

Mji wa Kano ambao una Waislamu wengi uko miongoni mwa Majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria ambayo yamepiga marufuku pombe chini ya sheria za Kiislamu.

Bia zilizoteketezwa zilikamatwa kutoka kwenye malori yaliyokuwa yakitoka eneo la kusini lenye Wakristo wengi……… hii sio mara ya kwanza kufanya hivi kwani Polisi wa eneo hilo mara kwa mara huharibu pombe na dawa za kulevya japo uharibifu huu umetia fora kwa sababu umekua mkubwa kuliko wakati mwingine.

Leave a Comment