
Kocha wa Asec Mimosas amesema wamejiandaa vizuri kukabiliana na Simba SC kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha huyo anasema wanajua Simba ni timu yenye uzoefu mkubwa na kikosi chenye ubora unaotakiwa kwenye michuano hii ya vilabu ila anaamini timu yake itapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.