×

Watoto 7 Wauawa Kwenye Shambulio la Anga

WATOTO saba wameuawa nchini Niger katika shambulio la anga la jeshi la Nigeria likiwalenga “majambazi”, wenye silaha mpakani mwa nchi hiyo.


Watano wengine walijeruhiwa katika shambulio hilo linaloonekana kufanywa kwa bahati mbaya, gavana wa eneo la Maradi nchini Niger amesema.

 

Gavana Chaibou Aboubacar alisema wanne waliuawa papo hapo na watatu walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitalini televisheni ya taifa ilisema shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Nachade.

Leave a Comment