
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, ameapa kuipambania Yanga katika mchezo unaofuata wa ligi kuu
dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi wakiwa ugenini.
Yanga katika mchezo huo, wanatarajiwa kuwa ugenini kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro, utakaochezwa keshokutwa Jumatano.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayele alisema kuwa licha ya kufahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu
lakini watapambana kama timu kuhakikisha wanaibuka na ushindi muhimu katika mchezo huo kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wenyewe.
“Tunafahamu ukubwa wa mchezo huu, ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi, hivyo tunatakiwa kuumaliza kwa ushindi, naona utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini lakini hatuhofii
hilo.
“Sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano na tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunaondoka na
ushindi, kila mchezo kwetu unahitaji ushindi, na hiyo ni kutokana na kuhitaji kutimiza malengo yetu msimu huu,” alisema Mayele.
Stori: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam