
Bunge la mpito nchini #Mali limepitisha kwa kura zote muswada wa kutawaliwa na jeshi kwa miaka mitano, licha ya vikwazo vilivyowekwa na ECOWAS kutokana na mchakato wa uchaguzi mkuu kucheleweshwa.
Awali, viongozi wa kijeshi waliahidi upigaji kura kuchagua viongozi utafanyika Februari, 2022 lakini ilipofika Desemba, 2021 mapendekezo ya jeshi kukaa madarakani kati ya miezi sita hadi miaka mitano yalitolewa, huku suala la usalama likitajwa kuwa sababu.
Mali iliingia katika utawala wa kijeshi baada ya mapinduzi yaliyofanyika Mei 2021. Jumuiya mbalimbali zinashinikiza utawala wa kiraia kurejeshwa nchini humo.