×

Trump Azindua Mtandao Wake wa Kijamii ‘Apple Store’

Aliyewahi kuwa rais wa Marekani Donald Trump amerejea na mtandao wake wa kijamii baada ya kupigwa marufuku Twitter

Jukwaa la mtandao huo unaojulikana kama Truth Social umezinduliwa kwenye programu ya Apple App store nchini Marekani.

Watumiaji wa awali walikutana na shida katika kusajili akaunti na baadhi ya wale wanaojaribu kujiandikisha walikuwa wakiambiwa ni kutokana na mahitaji makubwa.

Mtandao huo unafanana na Twitter na wachambuzi wanasema kuwa Trump alipigwa marufuku katika mitandao ya Twitter, Facebook na YouTube mwaka jana.

Leave a Comment