
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anawashutumu viongozi wa Ulaya kwa kutochukua hatua za kutosha kupunguza kasi ya Urusi kuvamia nchi yake.
Akizungumza kutoka ofisini kwake mjini Kyiv akiwa amevalia sare za kijeshi anasema, “Magari ya kivita na mashambulio ya angani ni sawa na kile Ulaya ilishuhudia wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia – kitu walichosema hakitawahi ‘kutokea tenane”.
Zelensky ameongeza kuwa bado hatujachelewa kukomesha “uchokozi” wa Urusi ikiwa viongozi wa Ulaya watachukua hatua haraka, na kutoa wito kwa raia kote Ulaya kuandamana na kushinikiza serikali zao kuchukua hatua madhubuti zaidi.