×

DC Jokate na ATE Waisafisha Kiburugwa Temeke

Februari 26, 2022 Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) wakimbatana na wanafunzi wa awamu ya Saba ya Programu ya Mwanamke Kiongozi (Female Future Programme) wameshirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo katika kusafisha eneo la Kiburugwa, Temeke.

 

ATE ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bi.Suzanne Ndomba-Doran wamekabidhi vifaaa vya kufanyia usafi kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bi Suzanne alisema “Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change) kwa kutunza mazingira na kusafisha mazingira yetu na kuunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dsm ma Serikali kwa ujumla, kampeni inayokwenda kwa jina la Safisha, Pendezesha Dsm “


Naye Raisi  wa wanafunzi wa Program ya wanawake awamu ya ya saba alitanabaisha kuwa “Kiongozi ni yule  anayatambua kuwa maendeleo yanachangiwa na usafi wa mazingira, pale mazingira yanapokuwa masafi huchagiza kuletwa kwa maendeleo kwenye jamii husika, sisi kama wanafunzi tunaohitimu masomo yetu ya Uongozi kwa Mwaka 2021-2022, tumejifunza na kutambua kuwa ili mafanikio yapatikane kwenye Jamii, kiongozi unatakiwa kufanya mabadiliko na kuwagusa kuanzia wananchi wa chini, kisha matokeo yataonekana na kuleta maendeleo hadi kwa wale waliopo juu, ndio sababu kwa kuanzia leo tumekuja kushirikiana na wakazi wa Temeke Kiburugwa kufanya usafi na kikabidhi vifaa vya usafi vitakavyo saidia kuendelea kutunza mazingira yetu ya sasa na ya baadae”.

 

Katika kuelekea Siku ya Mwanamke Duniani, chama cha waajiri Tanzania ATE kimeandaa Mkutano Wa Mwaka wa Uongozi utakaofanyika tarehe 2/3/2022 wenye Mada isemayo ”Usimamizi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi : Usawa kwa Maendeleo ya Sasa na Baadaye” ambao utaambatana na Mahafali ya Awamu ya Saba ya Programu ya Mwanamke Kiongozi.

Leave a Comment