×

Ukraine Yadai Kuna Vifo 4,300 Vya Warusi Mpaka Sasa

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Hanna Malyar ametoa makadirio ya hasara anayosema kuwa majeshi ya nchi hiyo yameisababishia Urusi hadi sasa.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Hanna amesema kwamba takwimu za siku tatu za kwanza za mzozo huo zilikuwa za awali na zinaweza kubadilika.

Ukraine inakadiria hasara za kijeshi za Urusi kufikia sasa kuwa ni pamoja na:

Vifo 4,300, kutunguliwa ndege 27, helikopta 26 na kuharibiwa kwa vifaru 146, magari 706 ya kivita, mizinga 49, mfumo mmoja wa ulinzi wa anga wa Buk, mifumo minne ya kurusha roketi nyingi za Grad, magari 30, meli 60 za mafuta, ndege zisizo na rubani (drone) mbili na boti 2.

Wakati huohuo, Ofisi ya Haki ya Serikali ya Ukraine ikiongozwa na afisa wake mkuu, Lyudmyla Denysova inasema zaidi ya raia 210 wa Ukraine wameuawa na zaidi ya 1,100 kujeruhiwa katika uvamizi wa Urusi.

“Kwa ukatili usioonekana, adui anaharibu majengo ya makazi, hospitali, shule za chekechea na shule, akichukua haki ya kuishi kutoka kwa watoto wa kiume na wa kike wa ardhi ya Ukraine,” alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii.

Denysova ametoa mifano ya baadhi ya vifo vya raia, ikiwa ni pamoja na mtoto aliyeuawa katika mashambulizi ya makombora katika hospitali huko Kyiv, na mwanamke aliyeuawa baada ya kombora kupiga jengo la makazi huko Kharkiv.

Ametoa wito kwa Urusi kuadhibiwa vikali kwa uhalifu huo.

Leave a Comment