
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, jana Jumapili amezindua mbio za Kilimanjaro Marathon zilizoanzia Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.

Baada ya uzinduzi huo Waziri Majaliwa alishiriki mbio za kilometa 5 na kuzimalizia kwenye uwanja huo.
Katika mbio hizo Aloyce Simbu wa hapa nchini Tanzania aliibuka mshindi wa kwanza huku wanawake Shelmith Muriuki kutoka Kenya ndiye aliyeibuka kidedea.


Katika mbio hizo kulukiwa na wakimbiaji wa kilometa 5 ambazo zinadhaminiwa na Grand Malt, kilometa 21 zinazodhaminiwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo na kilometa 42 ambazo zinadhamniniwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL