×

Championi, Spoti Xtra Yakabidhi Mifuko ya Mvua Kwa Mavenda

MAOFISA wa idara ya usambazaji wa Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Championi,Spoti Xtra na Ijumaa wikiendi iliopita walikabidhi mifuko ya plastiki kwa wauzaji wa magazeti ‘venda’ kwa ajili ya kufunikia magazeti katika kipindi hiki cha mvua.


Zoeeli hilo la kugawa mifuko hiyo lilisimamiwa na Francis Johanes na Mwanahamisi Khalid katika maeneo ya Sinza Palestina, Sinza Mori na Sinza Mapambano ikiwa na lengo la kuwasaidia mavenda hao kuyahifadhi magazeti katika meza wanazotumia katika kipindi hiki cha mvua ambazo zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Francis Johanes ambaye ni afisa usambaji wa Global Publishers amesema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu katika maeneo mbalimbali ikiwa na lengo la kuwasaidia wauzaji hao kufanya biashara yao katika mazingira mazuri bila ya kuharibu chochote katika kipindi hiki cha mvua.

Leave a Comment