
Baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Geita Gold FC jijini Mwanza, Young Africans SC ‘Timu ya Wananchi’ imerejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michezo mingine ya Ligi Kuu ya NBC.
Yanga SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wake Geita Gold FC na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara, NBC Premier League.
Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 42, na mechi zao mbili kabla ya kuivaa Simba ni KMC Machi 16, Dar, na Azam FC, Aprili 6, mwaka huu.