×

Live; Kiongozi wa Kijeshi wa Urusi Auawa Vitani, Yasema Ukraine

Kamanda wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa wakati wa mapigano karibu na Kharkiv, kulingana na wizara ya ulinzi ya ujasusi ya Ukraine.

Kulingana na taarifa kutoka wizara ya ulinzi ya Ukraine, Vitaly Gerasimov alikuwa jenerali mkuu, na naibu kamanda wa kwanza wa Jeshi la 41 la Wilaya ya Kati ya Kijeshi ya Urusi.

Idadi ya maafisa wakuu wa jeshi la Urusi pia waliuawa na kujeruhiwa, inasema.

Ujasusi wa Ukraine unasema Gerasimov alishiriki katika vita vya pili vya Chechnya na operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria. Alipokea medali “kwa kuirejesha Crimea”.

Maafisa wa Ukraine walituma picha ya mtu waliyesema kuwa ni Gerasimov kwenye ukurasa wa Twitter, yenye neno “Amefutwa” kwa herufi nyekundu chini kabisa.

Leave a Comment