
KAMPUNI ya bia ya Serengeti (SBL) inaendelea kuonyesha njia kwenye masuala ya kijinsia kwa kutoa fursa sawa kwa wanawake kwenye maeneo mbalimbali kama ajira, elimu, mapinduzi ya kilimo.
Napenda kusisitiza kuwa usawa siyo suala la wanawake, ni suala la kibiashara. Biashara yenye usawa ni biashara wezeshi. Usawa wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na jamii kuweza kusonga mbele,
”alisema Mark Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2022

Mkurugenzi huyo alisema kila mtu anawajibu wa kusaidia kuwepo kwa usawa wa kijinsia. Wote tunawajibika kwa mawazo na matendo yetu kila siku. “Tukiamua kupinga ubaguzi wa kijinsia tunaweza na tukafurahia kwa pamoja mafanikio ya wanawake.”
Mark alisema SBL katika programu zake inahakikisha kuwa ujumuishi wa makundi mbalimbali unakuwepo.

Kwa mfano katika programu yetu ya ufadhili wa masomo ya kilimo inayojulikana kama Kilimo Viwanda ambayo tumefadhili wanafunzi 200 mpaka hivi sasa, tumehakikisha kuwa uwakilishi wa nusu kwa nusu kati ya wanaume na wanawake unakuwepo,” alisema
Anasema pia SBL inaendesha program ya STEM ambayo huwachukua kutoka vyuoni vijana wa kike wanaofanya vizuri katika fani za sayansi, teknalojia pamoja na hisabati na kuwapa fursa ya kujifunza kwa vitendo kwa muda wa mwaka mmoja katika viwanda vyake.
“Tangu tuanzishe programu hii mwaka 2020, vijana wengi wa kike wameweza kupata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika idara zetu mbalimbali.
Lengo letu ni kuona mtoto wa kike anakuwa sehemu ya maendeleo ya sayansi kwa kunufaika moja kwa moja na fursa mbalimbali,” alisema.
Mark anasema SBL kupitia kampuni yake mama ya Diageo imekuwa ikihamasisha ujumuifu wa makundi mbalimbali katika shughuli zake ikilenga kuwa na uwakilishi wa nusu kwa nusu kati ya wanawake na wanaume kufikia mwaka 2030.