×

Tanzia: Rais Rupiah Banda Afariki Dunia

Aliyewahi kuwa Rais wa Zambia, Rupiah Banda amefariki dunia leo Ijumaa, Machi 11, 2022 akiwa na umri wa miaka 85.

Banda alikuwa akisumbuliwa na tatizo la saratani ya utumbo ambapo kwa mara ya kwanza aligundulika kuwa na ugonjwa huo mwaka 2020 baada ya kufanyiwa uchunguzi. Hayo yamesemwa na mtoto wake wa pili wakati akithibitisha kutokea kwa msiba wa baba yake.

“Baba amefariki majira ya saa 1:00 jioni, leo.” Amesema mtoto wa marehemu.

Banda ni Rais wa nne wa Zambia aliyechaguliwa kidemokrasia nchini humo na aliiongoza Zambia kuanzia mwaka 2008 hadi 2011.

Banda aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Zambia mwaka 2006 chini ya aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Levy Mwanawasa.

Baadaye mwaka 2008, Mwanawasa alipata stroke hivyo Banda akapewa jukumu la kuwa Rais wa mpito na miezi michache baadae, mwaka huo huo uchaguzi ulipofanyika alifanikiwa kushinda urais.

Mwaka 2013, bunge la nchi hiyo lilimuondolea Banda kinga ya kutoshitakiwa na kuruhusu mamlaka kumfanyia uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Hata hivyo hakuwahi kushitakiwa wala kufungwa kutokana na tuhuma hizo.

#RIPBanda

Leave a Comment