
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameshiriki katika mashindano ya mbio za magari ambayo yamefanyika katika uwanja wa Luzhniki ulioandaa mashindano ya fainali ya kombe la dunia la mwaka 2018, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa kura za maoni za Jimbo la Crimea.

Wakaazi wa Crimea wamepiga kura za maoni ambapo idadi kubwa ya wakaazi hao, wameunga mkono Crimea kuungana na Urusi.
Crimea ilikuwa chini ya utawala wa Ukraine kabla halijachukuliwa na Putin kwa nguvu mwaka 2014 na wakati raia hao wa Crimea wanapiga kura za maoni za kutaka kujiunga na Urusi, eneo hilo tayari lilikuwa limeshikiliwa na majeshi ya Urusi.

Katika tukio hilo Putin alipata nafasi ya kuhutubia wananchi waliohudhuria ambapo aliwapongeza raia wa Crimea ambao kwa sasa wanahesabika kama raia wa Urusi na kuwasifia wanajeshi wake ambao wanaendelea kutekeleza mapigano nchini Ukraine.