
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro eneo la Oilcom Nanenane.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Fortunatus Muslimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa Said Abdallah ambaye alikuwa dereva wa gari hilo pamoja na Ramadhan Muya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 hadi 35 ambaye alikuwa ni kondakta wa gari hilo.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa chanzo ni mwendokasi.