×

Uwoya apigwa miwani ya gharama

Irene Uwoya; ni mwanamama pisi kali ya Bongo Movies ambaye amejikuta akipigwa ile miwani yake ya bei mbaya huku watu wakihoji alipokuwa chawa wake, Aristote.

Katika video aliyoposti mwigizaji Anko Zumo ameonesha kuguswa na kitendo cha shabiki ambaye anaonekana akiiba miwani hiyo.

Shabiki huyo anaonekana akinyakua kwa nguvu miwani aliyokuwa ameivalia Uwoya.

Uwoya alikutwa na tukio hilo wakati akitaka kuonesha mapenzi kwa mashabiki wake.

Kwa mujibu wa Ako Zumo, hulka kama hizo ndizo zinazowafanya mastaa wengi kutochanganyikana kwa urahisi na mashabiki wao.

Ameandika; “Usipofungua kioo watasema unaringa, haya sasa kama hiyo miwani ilikuwa kwa ajili ya matatizo ya macho utamuuzia nani?”
Baadhi ya mashabiki na wasanii walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakiwataka mashabiki kuacha tabia za aina hiyo.

Pamoja na kwamba Uwoya hajazungumzia tukio hilo mpaka sasa, lakini alionekana kushtushwa na tukio hilo.
Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment